Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Cuba-Marekani: wakati wa historia wa kufungua upya balozi

media Wakati marais wawili, Barack Obama na Raul Castro wakipeana mikono mwezi Desemba mwaka 2013, miezi kadhaa ilikua imeshapita tangu mazungumzo kuhusu kufufua uhusiano wa nchi hizi kuanza. REUTERS/Kai Pfaffenbach

Jumatatu Julai 20, Marekani na Cuba zinatazamiwa kufufua rasmi mahusiano yao ya kidiplomasia. Mpaka sasa nchi hizi mbili zimekua bado na sehemu ya maslahi ya pamoja ikiwa katika mji wa Havana na washington.

Huu ni ukurasa mpya katika historia ya uhusiano wao ambaounafunguliwa, baada ya miaka 54 ya uadui.

Ilikuwa ni moja ya matukio ya mwisho ya vita baridi. Marekani na Cuba zilianza kuwa maadua tangu kuvunjika kwa mahusiano ya kidiplomasia mwezi Januari mwaka 1961, baada ya rais wa Marekani Dwight Eisenhower kuchukua uamzi.

Tangu ukuta wa Berlin kuanguka, rais Barack Obama alikubali kushindwa kwa sera za Marekani kwa Havana, na nchini Cuba , Raul Castro, aliyemrithi ndugu yake Fidel Castro, alianzisha hatua za ufunguzi wa sekta ya kiuchumi.

Wakati marais hawa wawili walipopeana mikono mjini Johannesburg mwezi Desemba mwaka 2013 wakati wa sherehe za mazishi ya Nelson Mandela, ilikuwa tayari miezi sita ambapo waliku walianza mazungumzo ya siri kwa kufufua uhusiano huu. Miezi kumi na nane ya mazungumzo na upatanishi yaliyokua yakisimamiwa na Vatican na mwezi Desemba 17 mwaka 2014, marais hawa wawili waliushangza ulimwengu kwa kutangaza kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa ya Marekani na Cuba.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFIVéronique Gaymard, ambaye yuko Havana, tangu mwezi Desemba, wajumbe wa Marekani na Cuba walikutana mara kadhaa. Jumatatu, Julai 20, sehemu za maslahi zitabadilishwa rasmi kwa balozi mjini Washington na Havana.

Ishara ya nguvu, hatua ya kwanza katika mchakato wa kuelekea kuhalalisha mahusiano ambayo yatachukua muda mrefu zaidi kwa kutatua migogoro kati ya nchi hizi mbili, kama vile kuondoa vikwazo viliombwa na Raul Castro. " Miongo kadhaa ya uadui haitoweka mara moja ", alisema mwezi Januari mwakilishi wa Idara ya Marekani Roberta Jacobson.

“ Kufufua mahusiano ya kidiplomasia ni jambo moja, kuhalalisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili itakuwa ngumu zaidi ”, amesema Stéphane Witowski mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mafunzo ya hali ya juu nchini Amerika ya Kusini (IHEAL).

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana