Pata taarifa kuu

Ban Ki-moon apongeza juhudi za kupambana na Ukimwi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kuwa dunia inaelekea kuwa na “ kizazi huru kisicho na maambikizi ya virusi vya Ukimwi ”.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa wafadhili wa maendelo , Adis Ababa, Julai 13 mwaka 2015.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa wafadhili wa maendelo , Adis Ababa, Julai 13 mwaka 2015. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na Ukimwi, UNAIDS limesema maambukizi yamepungua kwa asilimia 35 kidunia katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.

Habari hii ya chanya kuhusu kuelekea kizazi huru kisicho na maambukizi ya virusi vya UKIMWI, inatolewa huku pia wito ukitolewa kwa mataifa ulimwenguni kuingeza mchango wao wa kifedha kwa malengo ya kutokomeza kabisa virusi hivi ifikapo mwaka 2030, huku umoja wa mataifa ukionya kuwa kuendelea kuwanyanyapaliwa kwa watu wanaofanya biashara ya ngono, watumiaji wa dawa za kulevya na watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, ni sehemu ya kikwazo kuelekea malengo ya kuwa na kizazi huru kisichokuwa na maambukizi.

Wito huu wa kuchangia fedha zaidi unatolewa wakati huu ambapo mataifa mengi yanayoendelea yakikabiliwa na changamoto ya ukusanyaji wa fedha kusaidia watu walioathirika na virusi vya Ukimwi, ambapo nchi ya Tanzania ni miongoni mwa mataifa duniani yanayokabiliwa na changamoto hii.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNAIDS, inasema kuwa dunia imepiga hatua kubwa na kwamba imefikia malengo na hata kuvuka baadhi ya malengo kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi, ripoti iliyotolewa kwenye mkutano wa kimataifa unaoendelea mjini Addis Ababa Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.