Marais wa Marekani na Cuba watazamiwa kukutana
Mkutano wa Amerika, ambao unaanza Ijumaa wiki hii hii katika mji wa Panama, unaweza kuwa kama ulivyoelezwa wa kihistoria kwa sababu ni mara ya kwanza Cuba kushiriki mkutano huo.
Imechapishwa:
Inaarifiwa kuwa marais wa Marekani na Cuba wanatazamiwa kutana katika mkutano huo. Uhusiano kati ya Marekani na Cuba ulikua ulikatizwa kwa kipindi cha nusu karne, baada ya Marekani kuiwekeza Cuba vikwazo ikiituhumu kufadhili Ugaidi.
Siku chache baada ya rais wa Marekani Barack Obama kuthibitisha kufunguliwa kwa ubalozi wa nchi yake nchini Cuba kuanzia mwezi Aprili huu wa Aprili, hatimaye anatazamiwa kukutana kwa mazungumzo ya ana kwa ana na kiongozi wa nchi hiyo nchini Panama ijumaa wiki hii.
Mwanadiplomasia wa cheo cha juu wa Marekani katika nchi za Marekani ya kusini Roberta Jacobson, alisema kuwa itawezekana kufunguliwa kwa ubalozi kabla ya mkutano wa kimaeneo unaofanyika leo Ijumaa.
Mkuu wa ujumbe wa Cuba Josefina Vidal amesisitiza kuwa Marekani ni lazima iondoe Cuba kutoka kwa orodha ya nchi ambazo zinaunga mkono Ugaidi kabla ya kurejesha tena uhusiano huo.
Mwezi Disemba Cuba na Marekani walitangaza kuwa walikubaliana kuboresha uhusiano wao baada ya zaidi ya miaka 50.