Pata taarifa kuu
MAREKANI-SAUDI ARABIA-DIPLOMASIA

Barack Obama ziarani Saudi Arabia

Rais wa Marekani Barack Obama anakutana Jumanne Januari 28 na mfalme mpya Salman wa Saudi Arabia, baada ya kukamilisha ziara yake nchini India.

Baada ya India, Barack Obama, hapa akiwa New Delhi, anajielekeza Riyadh kwa ajili ya mazungumzo mafupi na mfalme Salman.
Baada ya India, Barack Obama, hapa akiwa New Delhi, anajielekeza Riyadh kwa ajili ya mazungumzo mafupi na mfalme Salman. REUTERS/Jim Bourg
Matangazo ya kibiashara

Obama anakutana kwa mazungumzo na mfalme Salman ili kujaribu kuboresha uhusiano wa nchi hizi mbili, baada ya uhusiano huo kuingiliwa na dosari kufuatia Marekani kubaini kwamba wengi miongoni mwa watu waliohusika na mashambulizi ya septemba 11 yalioitikisa nchi hiyo ni raia wa Saudi Arabia.

Hata hivyo nchi hizi mbili bado zina uhusiano wa karibu katika sekta mbalimbali.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI mjini Washington, Anne-Marie Capomaccio, Barack Obama hakuchelewa kukutana na mfalme Salman. Ziara ya Obama nchini Saudi Arabia ni rasmi kutokana na masuala ambayo yatakayo jadiliwa ni mengi, ikiwa ni pamoja na hali inayojiri wakati huu nchini Yemen, Iraq na Syria.

Kwa sasa Yemen inakabiliwa na mgogoro na vurugu, huku Iraq na Syria zikiwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, pamoja na Marekani kufanya mazungumzo na hasimu wake Iran. Hayo ni miongoni mwa masuala nyeti yatakao pewa uzito katika mazungumzo kati ya viongozi hao wawili.

Ikulu ya rais wa Marekani haitarajii mabadiliko katika mahusiano baina ya nchi hizo mbili, lakini kuna umuhimu mahusiano hayo yashughulkikiwe kwa kina. Mkakati wa Obama kwa Syria ilikuwa hauungwi mkono na Riyadh.

Saudi Arabia ilighadhibishwa na msimamo wa Marekani wa kutoingilia kati ili utawala wa Assad uondolewe. Na kama jeshi la Saudi Arabia lilishiriki katika vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam ni kufuatia uamzi uliochelewa wa kuwapa silaha waasi wa Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.