Pata taarifa kuu
MEXICO-Haki za binadamu-Usalama

Mexico: Marekani yaomba mwanga utolewe kuhusu kukosekana kwa wanafunzi

Serikali ya Marekani na Shirikisho la mataifa ya bara la Amerika wameiomba serikali ya Mexico kufanya kinachowezekana ili mwanga utolewe kuhusu wanafuzi 43 wa vyuo vikuu waliokosekana tangu kutokee shambulio liliyotekelezwa na polisi pamoja na kundi la wahuni siku kumi zilizopita kusini mwa Mexico.

Polisi inaendea kuzingira eneo kuliko gunduliwa makaburi sita ya pamoja karibu na mji wa Iguala..
Polisi inaendea kuzingira eneo kuliko gunduliwa makaburi sita ya pamoja karibu na mji wa Iguala.. REUTERS/Jorge Dan Lopez
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Wizara ya mashauri ya kigeni ya Marekani, Jen Psaki, amesema kukosekana kwa wanafunzi hao, ni uhalifu unaotia hofu, ambao unatakiwa uchunguzi wa kina, huku akiomba wahusika wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Hata hivo, akiongea akiwa ziarani Washington, Katibu mkuu wa Shirikisho la mataifa ya bara la Amerika, José Miguel Insulza, ameelezea wasiwasi wake juu ya uhalifu huo.

Vitendo vya kikatili vimekua vikishuhudiwa mara kwa mara nchini Mexico bila hata hivo kuadhibu wahalifu, lakini kugundulika hivi karibuni kwa makaburi sita ya pamoja kumezua utata katika serikali.

Jumatatu wiki hii kikosi cha wanajeshi pamoja na kikosi cha askari polisi wa usalama wa raia kilichukua udhibiti wa eneo hilo na kuamua kuwapokonya sialaha askari polisi wa mji wa eneo kulikogunduliwa makaburi, huku idadi ya wanajeshi ikiendelea kuongezwa.

Septema 26 mwaka 2014 kulishuhudiwa makabiliano makali katika mji huo wa Iguala uliyo kwenye umbali wa kilomita 200 kusini mwa Mexico, wenye wakaazi 140,000. Makabiliano hayo yalikua kati ya polisi na wanafunzi waliokua wamekuja, kulingana na kauli zao, kukusanya pesa kwa ajili ya visomo vyao.

Polisi imekua ikinyooshewa kidolea kwamba ilishirikiana na kundi la wahuni (Guerreros Unidos) kwa kuwashambulia kwa risase wanafunzi hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.