Pata taarifa kuu
IRAQ-MAREKANI-ISIL-Usalama

Iraq : mwandishi wa habari, raia wa Marekani achinjwa

Makundi ya kislamu yanayoshikilia baadhi ya maeneo nchini Iraq na Syria yamemua mwandishi wa habari, raia wa Marekani, James Foley, yakieleza kwamba ni kujibu mashambulizi ya Marekani, ambayo ilianzisha hivi karibuni dhidi ya ngome za wapiganaji wa makundi hayo.

Mknda wa video unaoonesha namna mwandishi wa habari James Foley akiuawa kwa kuchinjwa.
Mknda wa video unaoonesha namna mwandishi wa habari James Foley akiuawa kwa kuchinjwa. REUTERS/Social Media Website via REUTERS TV
Matangazo ya kibiashara

James Foley alitekwa nyara tangu miaka miwili iliyopita nchini Syria. Makundi hayo ya kislamu yametishia kuua raia mwengine wa Marekani, ambayo yanamshikilia.

Foley ameoneshwa katika mkanda wa video akiuawa kwa kuchinjwa na mmoja wa wapiganaji hao wa kislamu ambaye amekua ameficha uso, huko akitishia kuua mwanahabari mwengine kutoka Marekani, ambaye pia ameoneshwa katika mkanda huo wa video unaodumu dakika tano.

Mpiganaji huyo amesema mwandishi huyo wa Marekani atauawa kama jinsi alivyouawa Foley, iwapo Barack Obama hatositisha harakati zake za kuendesha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa kislamu nchini Iraq. Jeshi la Marekani linaendelea na mashambulizi dhidi ya makundi hayo ya kislamu katika mji wa Tikrit, baada ya makundi hayo kupoteza eneo muhimu la Mossoul.

James Foley ni mwandishi wa habari mwenye uzowefu mkubwa, ambaye alifanya kazi yake wakati wa vita vya Afghanistan na nchini Iraq. Foley aliwahi kukamatwa mateka pia kwa muda wa majuma 6 nchini Libya.

Familia ya mwandishi huyo wa habari imethibitisha kifo chake, huku Marekani ikijizuia kutoa taarifa yoyote inayohusiana na kifo hicho.

Hayo yakijiri, jeshi la anga la Marekani limeanzisha mashambulizi ya anga katika mji wa Tikrit. Mashambulizi hayo ni ya pili baada ya kuwatimua wapiganaji wa makundi ya kislamu katika eneo mhimu kunako patikana bwawa linalozalisha umeme wa kiwango kikubwa nchini Iraq katika jimbo la Mossoul.

Hata hivo wapiganaji hao wanaonekana wana mafunzo ya kutosha na wana silaha za kisasa kuliko majeshi ya Iraq, kwani baada ya jeshi la Iraq na wapiganaji wa kikurdi kuteka eneo la Chichine kusini magharibi mwa Iraq wakisaidiwa na jeshi la anga la Iraq, wanajeshi hao na wapiganaji wa kikurdi wameanza kujiondoa katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.