WHO yautaja ugonjwa wa Corona kama 'adui wa kwanza kwa umma'
Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kwamba ugonjwa unaofahamika kama Corona, ambao hatimaye unaitwa "Covid-19" ni "tishio kubwa kwa ulimwengu mzima" na unapaswa kuchukuliwa na jamii ya kimataifa kama "adui wa kwanza kwa umma".
Imechapishwa:
Akiongea kwenye semina iliyohudhuriwa na watafiti zaidi ya 400 na wawakilishi wa mamlaka za afya za kitaifa huko Geneva, mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa wito wa kugawana sampuli za virusi na kuongeza kasi kwa kutafuta matibabu na chanjo.
"Wakati 99% ya visa vya virusi hivyo vinatokea nchini China, bado hali hii inasalia kuwa janga la dharura kwa nchi hiyo, lakini pia na kutoa kitisho kikubwa kwingineko duniani", Tedros Adhanom Ghebreyesus amebainisha.
🚨 BREAKING 🚨
World Health Organization (WHO) (@WHO) February 11, 2020
"We now have a name for the #2019nCoV disease:
COVID-19.
I’ll spell it: C-O-V-I-D hyphen one nine – COVID-19"
-@DrTedros #COVID19 pic.twitter.com/Kh0wx2qfzk
Virusi hivyo vilivyotambulika kwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan Desemba 31, vimeuwa zaidi ya watu 1,000, na zaidi ya watu 42,000 wameambukiwza virusi vya ugonjwa huo na kusambaa katika nchi 25.