Pata taarifa kuu
CHINA-WHO-AFYA

Ugonjwa hatari wa Corona waua zaidi ya watu 1,000 nchini China

Idadi ya vifo vinavyosababishwa na mlipuko wa ugonjwa mpya unaofahamika kama Corona imefikia 1,000 leo Jumanne. kwa upande mwengine shirika la Afya Duniani (WHO), limesema idadi kubwa ya visa vya maambukizi nje ya nchi hii inaweza kuzidisha kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo duniani.

Rais wa China, Xi Jinping leo amewatembelea wagonjwa wa virusi vya Corona pamoja na maafisa wa afya ambao wanawahudumia wagonjwa hao.
Rais wa China, Xi Jinping leo amewatembelea wagonjwa wa virusi vya Corona pamoja na maafisa wa afya ambao wanawahudumia wagonjwa hao. (Foto: AFP/XINHUA / JU Peng)
Matangazo ya kibiashara

Hivi karubuni shirika la Afya Duniani (WHO) lilipeleka ujumbe wa wataalam nchini China kushirikiana na maafisa wengine wa afya kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.

Kifo cha kwanza kilichotokana na virusi vya 2019-nCoV, ambavyo viligunduliwa mwezi Desemba katika mji wa katikati mwa China wa Wuhan, vilitangazwa Januari 11. Mwezi mmoja baadaye, ugonjwa huo sasa umeuwa watu 1,016 kwa China pekee (ukiondoa Hong Kong na Macao), kulingana na ripoti rasmi iliyochapishwa Jumanne.

Maafisa wa afya nchini China wameripoti vifo vipya 108 ndani ya saa ishirini na nne, ikiwa ni idadi kubwa zaidi tangu kuzuka kwa ugonjwa huo, wakati kesi za maambukizi zikifikia zaidi ya 42,000.

Kwa upande mwingine, tangu wiki iliyopita, idadi ya kesi mpya za kila siku (2,478) imepungua ikilinganishwa na siku iliyopita.

Jumatatu wiki hii rais wa China Xi Jinping alitoa wito wa kuchukuliwa "hatua kali zenye maamuzi ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa" baada ya kutembelea eneo la makazi la Beijing kuzuru hospitali mmoja, ambapo alionekana kwa mara ya kwanza amevalia kitambaa cha kufunika uso kwa ajili ya kujikinga na pia alipima afya yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.