Pata taarifa kuu
NIGERIA-LASSA-AFYA

Homa ya Lassa yaua arobaini na mmoja Nigeria

Watu 41 wamepoteza maisha nchini Nigeria kwa muda wa mwezi huu wa Januari kutokana na homa ya Lassa, katika majimbo mbalimbali nchini humo.

Hospitali ya Ibadan, mji mkuu wa Jimbo la Oyo, Nigeria.
Hospitali ya Ibadan, mji mkuu wa Jimbo la Oyo, Nigeria. wikimedia/cc
Matangazo ya kibiashara

Shirika linaloshughulikia udhibiti wa magonjwa nchini humo linasema mbali na vifo hivyo, kati ya tarehe 1 na 26 mwezi huu watu wengine 258 wameambukizwa.

Miongoni mwa watu walioambukizwa ni pamoja na wafanyikazi watano wa afya katika majimbo 19.

Maambukizi ya Lassa yanafanan na yale ya Ebola na Marburg, lakini sio hatari sana, kwa mujibu wa watalaam wa afya.

Ugonjwa huo huambukizwa kwa kugusa kinyesi cha panya na mkono na dalili zake ni kupanda kwa joto mwilini, na kutokwa damu katika maeneo yaliyo wazi.

Tangu kutangazwa kwa homa hii mwaka 2019, watu 170 wamepoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.