Pata taarifa kuu
DRC-SURUA-AFYA

UN: Surua yaua watu 6,000 DRC

Shirika la afya ulimwenguni, WHO, limetoa wito wa kuongezwa kwa msaada wa kimataifa katika kupambana na ugonjwa hatari wa Surua unaoambukiza kwa kasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Ugonjwa wa surua unaendelea kuikumba DRC.
Ugonjwa wa surua unaendelea kuikumba DRC. AFP PHOTO / LIONEL HEALING
Matangazo ya kibiashara

Ombi hilo limekuja wakati huu ambapo idadi ya waliokufa kutokana na surua imevuka watu 6,000.

Hata hivyo, katika maeneo mengine, idadi ya waliopokea chanjo inasalia kuwa ndogo ikiwa ni asilimia 25 ya visa vya surua vilivyoripotiwa ni miongoni mwa watoto waliozidi umri wa miaka mitano ambao wako hatarini zaidi.

Tangu mwanzo wa mwaka 2019, takriban watu 310,000 waliripotiwa kuwa na surua.

Mriipuko huo ulisababishwa na viwango vya chini vya chanjo, mfumo mbaya wa afya, utapiamlo na ugumu wa kufikia jamii zilizo hatarini na huduma ya afya kwa sababu za kiusalama.

Desemba 2019, WHO ilitoa mafunzo kwa wauguzi 60 kutoka wizara ya afya kwa ajili ya kuendesha program ya ushirika wa jamii, elimu ya afya na ufuatiliaji ambapo wauguzi hao wanasaidia katika kukabiliana na hali ya sasa.

WHO, muungano wa chanjo ulimwenguni, GAVI na wadau wengine walitoa chanjo kwa zaidi ya watoto milioni 18 walio chini ya umri wa miaka mitano kote nchini DRC mwaka 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.