Pata taarifa kuu
BRAZILI-MAJANGA YA ASILI

Moto waendelea kuharibu mali Amazon

Moto wa misitu Amazon, nchini Brazili umeongezeka zaidi ndani ya saa 24 zilizopita, siku ya pili ya operesheni za jeshi la nchi hiyo za kukabiliana dhidi ya moto huo, wakati nchi zilizostawi kiuchumi duniani (G7) zilitangaza Jumatatu kutoa msaada wa dharura.

Msitu wa Amazon unaendelea kuteketea kwa moto.
Msitu wa Amazon unaendelea kuteketea kwa moto. REUTERS / Bruno Kelly
Matangazo ya kibiashara

Kesi mpya 1,113 za moto ziliorodheshwa siku ya Jumapili nchini Brazili na Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti (INPE). Kwa jumla, kesi karibu 80,000 za moto wa misitu zimeorodheshwa nchini Brazili tangu mwanzoni mwa mwaka huu - kiwango cha juu zaidi tangu 2013 - zaidi ya nusu iliorodheshwa katika msitu wa Amazon.

Hata hivyo siku ya Jumatatu Waziri wa Ulinzi wa Brazili alisema kuwa moto wa Amazon "umedhibitiwa udhibitiwa" baada ya kupelekwa kwa askari zaidi ya 2,500 na mvua kuripotiwa katika maeneo kadhaa yaliyoathirika.

Hali hiyo "iliongezeka," ameongeza Fernando Azevedo e Silva, ambaye aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano na Rais Jair Bolsonaro kwamba Brazil ilipitia wakati mgumu ya "mikasa ya moto wa kiwango cha juu" katika miaka iliyopita miaka.

Katika Jimbo la Rondônia (kaskazini-magharibi mwa Brazili), kwenye mpaka na Bolivia, mji wa Porto Velho uliendelea kufunikwa na mawingu makubwa ya moshi siku ya Jumatatu, licha ya jeshi kuendelea na operesheni zake za kukabiliana na moto huo tangu siku ya Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.