Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afya - Mazingira

OCHA: Ugonjwa wa Malaria umekuwa sugu Burundi

media Anopheles ndio mbu kuu inayoambukiza virusi vya ugonjwa wa Malaria kwa wanadamu. Getty Images

Nchi ya Burundi inaendelea kukumbwa na ugonjwa wa Malaria ambao hivi karibuni serikali imekuwa ikijitahidi kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuhimiza wananchi kutumia vyandarua.

Mtu mmoja kati ya watu wawili anaugua ugonjwa wa malarianchi Burundi, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya matabibu. Zaidi ya visa milioni 5.7, pamoja na vifo 1,801, vimeripotiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi tarehe 21 Julai 2019, kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa OCHA, kwa jumla ya wakaazi milioni 11 nchini humo. Serikali ya Burundi haijatangaza rasmi Malaria kama janga linaloikabili nchi hiyo, licha ya mashirika kadhaa ya kimataifa kuomba ugonjwa wa Malaria kutangazwa kama janga.

Kuanzia milioni tatu mnamo mwezi Mei, idadi ya kesi za ugonjwa wa Malaria nchini Burundi ziliongezeka hadi zaidi ya milioni 5.7 katikati ya mwezi Julai, kulingana na takwimu zilizochapishwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA nchini humo. Shirika hili la Umoja wa Mataifa limenukuu data rasmi kutoka kwa Wizara ya Afya ya Burundi.

Ni idadi kubwa ya wananchi wa Burundi kwa jumla ya wakaazi milioni 11 ambao tayari wameathiriwa na mlipuko huu mpya wa ugonjwa wa Malaria kwa zaidi ya siku 200, ikimaanisha kuwa ugonjwa huo umeongezeka kwa asilimia 97 kwa kipindi kama hicho cha mwaka 2018.

Watu takribani 1,800 wamefariki dunia na ugonjwa huu katika kipindi hicho na hiyo ni ishara kwamba ugonjwa huo bado haujadhibitiwa. Zaidi ya kesi 150,000 mpya - pamoja na vifo 65 - vimeorodheshwa kwa wiki moja pekee, kuanzia Julai 15 hadi 21, kulingana na ripoti ya OCHA.

Tatizo kubwa leo ni kwamba serikali ya Burundi inakataa kutangaza rasmi janga la ugonjwa wa malaria, licha ya ombi kutoka kwa mashirika ya kimataifa katika mwelekeo huu tangu katikati ya mwezi Aprili.

Katika miongo kadhaa iliyopita juhudi za kupambana na ugonjwa wa malaria ziliimarika, lakini tangu mwaka 2015 juhudi hizo zimeonekana kutetereka.

Ripoti mpya ya WHO kuhusiana na hali ya malaria duniani (iliyotolewa mwaka 2018) inaashiria kuwa viwango vya maambukizi havijashuka kati ya 2015 mwaka 2017.

Ugonjwa huo unaua mtoto mmoja kila baada ya dakika mbili huku visa vipya zaidi ya milioni 200 vikiripotiwa kila mwaka, kwa mujibu wa Data za Shirika la Afya Duniani(WHO).

Malaria ni ugonjwa ambao una tiba lakini unaendelea kusababisha vifo vingi duniani.

Malaria ni ugonjwa hatari unosababishwa na vimelea aina nne: P. falciparum, P. malariae, P. ovale na P. vivax.

Vimelea hao huingizwa ndani ya mwili wa binadamu na mbu wa kike wanaofahamika kama Anopheles wanapomuuma mtu.

Ugonjwa huo unaweza kukingwa na pia kutibiwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana