Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFY

DRC na majirani zake waendelea kukabiliana na kuenea kwa Ebola

Wakati huu wafanyakazi wa afya wakiendelea na juhudi za kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Ebola Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuna hofu kuwa kutokuwepo kwa utashi wa kisiasa kutasababisha ugonjwa huu kuenea pakubwa.

Kwenye mpaka na DRC, katika eneo la Mpondwe, kumewekwa mabango yanaonya dhidi ya hatari ya Ebola, Juni 13, 2019.
Kwenye mpaka na DRC, katika eneo la Mpondwe, kumewekwa mabango yanaonya dhidi ya hatari ya Ebola, Juni 13, 2019. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Licha ya shirika la afya duniani WHO kutangaza ugonjwa wa Ebola mashariki mwa DRC kuwa janga la kidunia, jumuiya ya kimataifa imeshindwa kutoa fedha za kutosha kusaidia juhudi za kuzuia maambukizi, suala ambalo hata mkuu wa kitengo cha misaada ya kibinadamu cha umoja wa Mataifa Mark Lowcock anakiri.

Haya yanajiri wakati huu serikali Jimboni Kivu Kaskazini ikiweka mikakati thabiti ya kuhakikisha hakuna wagonjwa wapya wanaoripotiwa kwenye mji wa Goma na Beni.

Wakati huo huo serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeanza operesheni ya kutoa chanjo ya ugonjwa wa Ebola kwa wahudumu wa afya wakiwemo manesi na madaktari jimboni Kivu Kusini, chanjo ambayo ni sehemu ya juhudi ya Serikali kukabiliana na kuenea kwa maambukizi zaidi ya virusi vya ugonjwa huo.

Tayari nchi kadhaa zinazopakana na DRC ikiwemo Uganda, Tanzania, Kenya, Rwanda na Sudan Kusini zimeanza kuchukua tahadhari kwenye maeneo ya mipaka kutokana na tisho kubwa la kuenea kwa maambukizi zaidi.

Zaidi ya watu 1600 wamekufa tangu mwezi Agosti mwaka uliopita, kutokana na ugonjwa huo ambao ni wa pili kwa kuua watu duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.