Pata taarifa kuu
DRC-WHO-EBOLA-AFYA

Vita dhidi ya Ebola: DRC yaahidi kushirikiana na majirani zake

Wakati Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza mlipuko wa homa ya Ebola nchini Congo kuwa dharura ya kimataifa ya afya ya umma inayotia wasiwasi, serikali ya DRC imeahidi kushirikiana na majirani zake kupambana na Ebola.

Maafisa wa afya wakisafirisha mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya Ebola katika kituo cha matibabu cha Ebola cha Butembo, Novemba 4, 2018.
Maafisa wa afya wakisafirisha mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya Ebola katika kituo cha matibabu cha Ebola cha Butembo, Novemba 4, 2018. Photo: John Wessels/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii inakuja siku chache baada ya Shirika la la Afya Duniani (WHO) kuesema kuwa mvuvi wa kutoka DRC aliefariki kutokana na Ebola, huenda alibeba virusi kutoka Congo hadi ndani ya Rwanda na pia Uganda.

Akizungumza mbele ya vyombo vya habari mjini Goma, waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Dkt. Oly Ilunga, amesema nchi yake itafanya mazungumzo ya pamoja na nchi jirani kuhusu mbinu na mikakati ya kupambana na mlipuko wa Ebola katika eneo hilo.

Zaidi ya watu 1600 wamekufa tangu mwezi Agosti mwaka uliopita, kutokana na ugonjwa huo ambao ni wa pili kwa kuua watu duniani.

Hata hivyo Dkt. Ilinga amelaani kile alichokiita kuwa usambazaji wa taarifa zisizosahihi kupitia mitandao ya kijamii, kuhusu mlipuko wa ugonjwa huo.

Katika mkutano na vyombo vya habari mjini Goma Dkt. Ilunga ameelezea kuridhishwa na hatua ya shirika la Afya Duniani WHO, kuutangaza mlipuko wa sasa wa Ebola kuwa dharura ya kimataifa, baada ya mkutano uliofanyika mjini nchini Uswisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.