Pata taarifa kuu
DRC-PINDUPINDU-AFYA

Watu 125 wafariki dunia kufuatia mlipuko wa kipindupindu Kasai, DRC

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umesababisha vifo vya watu 125 tangu mwezi Februari huko Kasaï, katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, nchi ambayo tayari imekumbwa na milipuko miwili ya ugonjwa hatari wa Ebola mwaka huu.

Kituo cha matibabu dhidi ya ugonjwa w kipindupindu kilichojengwa na shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) nchini DRC.
Kituo cha matibabu dhidi ya ugonjwa w kipindupindu kilichojengwa na shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) nchini DRC. LIONEL HEALING / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kwa jumla wagonjwa 2,100 wanapewa matibabu, na tangu mwezi Februari tumeorodhesha vifo 125," Waziri wa Afya wa mkoa wa Kasai Mashariki, Hippolyte Mutombo Mbwebwe, aliimeliambia shirika la habari la AFP.

Maeneo ya madini ya almasi yanaendelea kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu Kasaï Mashariki, amesema.

Matukio mengine kumi, ikiwa ni pamoja na vifo viwili, yamethibitishwa katika mkoa jirani wa Kasai.

Mtu mmoja anayeshukiwa kuambukizwa ugonjwa huo amelazwa katika hospitali kuu ya mkoa, huko Kananga.

Hayo yanajiri wakati ambapo ugonjwa hatari wa Ebola unaendelea kukumba nchi hiyo kubwa tajiri kwa madini mbalimbali ya Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.