Pata taarifa kuu
JAPANI-DRC-EBOLA-AFYA

Japani yatenga dola 700,000 kwa ajili ya kupambana na Ebola DRC

Japani imetenga dola 700,000 kwa Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Watoto (Unicef) ili kukabiliana na virusi vya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako hakujaripotiwa kesi mpya ya mtu aliyefariki au maambukizi mapya ya Ebola kwa siku kadhaa.

DRC yaendelea kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola.
DRC yaendelea kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola. AFP Photo/Junior D. Kannah
Matangazo ya kibiashara

"Serikali ya Japani imetenga dola 700,000 kwa Unicef" ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola unaoathiri DRC, Japani imesema katika taarifa yake.

Fedha hizi "zitatumika kusaidia shughuli katika nyanja ya mawasiliano katika jamii na msaada wa kisaikolojia kwa familia zilizoathirika," Unicef imesema.

"Msaada wa Japani utatusaidia kuendelea kwa shughuli zetu kwa kuwapokea wagonjwa na kukomesha kuzuka kwa virusi vya Ebola hivi karibuni," amesema Dk. Gianfranco Rotigliano, mwakilishi wa UNICEF nchini DRC.

Mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola ulizuka Mei 8 kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, huko Bikoro, karibu na mpaka na Congo-Brazzaville, kilomita 100 kutoka mji mkuu wa mkoa wa Mbandaka na kilomita 600 kutoka mji wa Kinshasa.

Tangu wakati huo, watu 28 wamefariki dunia, kulingana na ripoti rasmi. Hakuna kesi mpya iliyotangazwa tangu siku kadhaa zilizopita.

Tangu uzinduzi wa zoezi la kutoa chanjo mnamo Mei 21, watu 3,139 wamepewa chanjo nchini DRC, kulingana na Wizara ya Afya ya DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.