Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afya - Mazingira

Watu 12 wapoteza maisha kutokana na Kipindupindu Nigeria

media Wakazi wa Adamawa wanawasiwasi ya kuongezeka kwa vifo vya watu kutokana na ugonjwa wa Ebola. REUTERS

Watu kumi na wawili wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa maradhi ya Kipindupindu katika jimbo la Adamawa, Kaskazini-Mashariki mwa Nigeria, waziri wa afya wa jimbo hilo amesema.

Mlipuko huu mpya, ulioanza siku ya Jumapili, umeathiri watu 142 katika wilaya ya Mubi, Ahmad Sajo ameliambia shirika la habari la AFP.

"Tumeorodhesha vifo 12 kutokana na mlipuko wa maradhi ya Kipindupindu katika wilaya ya Mubi Kaskazini na Mubi Kusini kwa muda wa siku nne zilizopita," Waziri Sajo amesema.

"Jumla ya watu 142 waliambukizwa na timu za matabibu zimetumwa kuhudumia watu hao ambao tayari wameshaambukizwa ili kudhibiti maambukizi ya haraka ya ugonjwa huo," ameomgeza.

Amesema kuwa timu za matabibu bado hazijagundua sababu ya ugonjwa huo. Ugonjwa wa Kipindupindu ambao unaambukia kwa njia ya matumizi ya maji yalijaa virusi vya ugonjwa huo husababisha kuhara, na watoto ndio wako hatari kubwa ya maambukizi.

Magonjwa yanayotokana na maji ni tishio la mara kwa mara kutokana na ukosefu wa vifaa vya usafi kwa mazingira na madimbwi ya maji yanayokaa kwa kipindi kirefu wakati wa msimu wa mvua nchini Nigeria.

Mwezi uliopita, watu 13 walifariki dunia kutokana na mlipuko wa ugonjwa unaofanana na kipindupindu katikaJimbo jirani la Yobe.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana