Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afya - Mazingira

Mvua zaua watu zaidi ya 78 nchini India

media kijiji kidogo cha jimbo la Rajasthan, India ambapo watu zaidi ya 78 wamepoteza maisha kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Vincent Desjardins

Mvua kubwa zimeua watu wasiopungua 78 kaskazini na magharibi mwa India, serikali ya nchi hiyo imetangaza. Watu wengi wamepoteza makazi yao kutokana na mvua hizo zinazoendelea nchini humo.

Watu thelathini na watatu walipoteza maisha siku ya Jumatano wiki hii katika jimbo la magharibi la Rajasthan na wengine 45 walipoteza maisha katika jimbo la Uttar Pradesh, kaskazini mwa nchi.

"Tumekumbwa na mvua kubwa yenye upepo usio wa kawaida hali ambayo ilisababisha watu 33 kupoteza maisha katika maeneo ya Alwar, Dholpur na Bharatpur, katika jimbo la Rajastan" amesema Hemant Gera, Afisa wa Idara ya huduma za dharura katika jimbo la Rajasthan.

Mvua hizo pia zimeathiri maeneo ya Saharanpur, Bareilly, Bijnore na Agra katika jimbo la Uttar Pradesh.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana