sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Mazungumzo ya amani kuanza Sudan, rais …
Rais wa DRC Felix Tshisekedi akiwa na mwenyeji wake rais wa Tanzania John Magufuli. 13 Juni 2019
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/06 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/06 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/06 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afya - Mazingira

Marekani kurejea kwenye mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Paris

media "Muisaidie", sayari: ujumbe uliotumwa wakati wa maandamano kwa niaba ya marais na viongozi wa serikali waliohudhuria mkutano kuhusu tabia nchi, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York. REUTERS/Carlo Allegri

Rais wa Marekani Donald Trump hapo amesema nchi yake huenda ikarejea kwenye mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Paris licha ya kutoweka wazi nia yake hasa ya kurejea kwenye makubaliano hayo.

Rais Trump amesema binafsi hana matatizo na makubaliano yaliyofikiwa lakini tatizo lake ni makubaliano yaliyotiwa saini akisema mara zote viongozi wa dunia wamekuwa wakikubaliana mikataba mibaya.

Mwezi Juni mwaka jana rais Trump alieleza nia ya kuiondoa nchi yake kwenye makubaliano ya Paris akisema mkataba uliotiwa saini na mtangulizi wake unainyima fursa Marekani kuwa taifa lenye nguvu.

Wataalamu wanasema mchakato wa nchi hiyo kujitoa kwenye makubaliano hayo utachukua muda na una vipengele vigumu hali inayoibua maswali ikiwa rais Trump alimaanisha kile alichokisema kuhusu kujitoa katika mkataba uliotiwa saini mwaka 2015.

Akiwa na mgeni wake waziri mkuu wa Norway Erna Solberg rais Trump amejisifu kama mpenda mazingira huku akijua madhara ya kidunia yatakayotokea ikiwa nchi yake itajitoa kwenye makubaliano ya Paris kupunguza hali ya joto la dunia.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana