Pata taarifa kuu
DRC-MAJANGA ASILI

Serikali ya DRC yaahidi kuwasaidia waathirika wa mvua mjini Kinshasa

Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo wanamalizia siku mbili za maombolezo ya kitaifa, kuwakumbuka watu 44 walipoteza maisha baada ya mvua kubwa kusababisha mafuruko na maporomoko ya udongo jijini Kinshasa wiki iliyopita.

Maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha Januari 5, 2019 Kinshasa, DRC.
Maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha Januari 5, 2019 Kinshasa, DRC. AFP/John Wessels
Matangazo ya kibiashara

Makaazi ya watu katika mitaa mbalimbali imeharibika na kusababisha mamia ya watu kukosa sehemu ya kuishi.

Changamoto hii ya mafuriko imeendelea kushuhudiwa kila mwaka, na kuharibu barabara za jijini.

Mbali na maafa hayo na makaazi ya watu kuharibika, kuna hofu kuwa janga hilo huenda likazua ugonjwa hatari wa kipindupindu.

Waziri Mkuu Bruno Tshibala alizuru mitaa iliyoathirika zaidi na kuahidi msaada wa serikali kuwasaidia waliopoteza makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.