Pata taarifa kuu
UFARANSA-KIPINDUPINDU-AFYA

Mkutano wa kumaliza kipindupindu kufanyika Ufaransa

Mkutano wa kumaliza kipindupindu ifikapo 2030 unaowajumuisha maafisa kutoka nchi mbalimbali duniani unafanyika nchini Ufaransa.

Eneo la Pakadjuma, Mkoa wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo: Wahamasishaji wa kijamii wanaweka vibango kuhusu hatua muhimu za kuepuka kipindupindu katika eneo la Pakadjuma lililoathiriwa na janga la kipindupindu.
Eneo la Pakadjuma, Mkoa wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo: Wahamasishaji wa kijamii wanaweka vibango kuhusu hatua muhimu za kuepuka kipindupindu katika eneo la Pakadjuma lililoathiriwa na janga la kipindupindu. Photo OMS/Eugene Kabambi
Matangazo ya kibiashara

Ugonjwa wa Kipindu pindu katika karne ya 21 umeelezewa kama ''aibu kubwa kwa dunia,"

Kipindupindu ni ugonjwa ambao unasambaa kupitia maji machafu na unau karibu watu 100,000 kila mwaka.

Si ghali kutibu ugonjwa huo na unaweza kuepukika kabisa ikiwa watu watapata maji safi na vyoo visafi.

Tayari ugonjwa wa kipindupindu ulitokomezwa nchini Uingereza na Marekani zaidi ya miaka 100 iliyopita, lakini unaendelea kusababisha vifo katika mataifa mengi yanayoendelea, hasa barani Afrika na nchi nyingi katika bara la Asia.

Maafisa kutoka kote duniani wanakutana nchini Ufaransa kujaribu kutafuta njia za kuzuia kwa asislimia 90 ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa kipindupindu ifikapo 2030.

Hii inakuja wakati Yemen inandelea kupambana na moja ya milipuko mibaya zaidi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.