Pata taarifa kuu

Watu 12 wafariki dunia kufuatia mlipuko wa ugonjwa usiojulikana Nyiragongo

Watu 12 wamepoteza maisha baada ya kuanza kuharisha na na kutapika katika kijiji cha Kanyaruchinya eneo la Nyiragongo katika Jimbo la Kivu Kaskazini.

Maji safi yamekua haba katika baadhi ya vitongoji vya mji wa Goma.
Maji safi yamekua haba katika baadhi ya vitongoji vya mji wa Goma. Stéphanie Aglietti/RFI
Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya kiraia yanasema miongoni mwa watu hao walipoteza maisha kuanzia siku ya Ijumaa ni watito saba wenye chini ya umri wa miaka mitano na watu wazima watano.

Watu wengine 120 wamelazwa hopsitalini mjini Goma, wanakopewa matibabu.

Ukosefu wa maji safi ya matumzi ya nyumbani katika maeneo mengi ya jimbo la Kivu Kaskazini, inaelezwa kuwa chanzo cha hali hii.

Serikali ya mjini Goma haijaeleza lolote kuhusu hali hii inayoendelea kushuhudiwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.