Pata taarifa kuu
WHO-AFYA-MALARIA

Dunia yaadhimisha siku ya Malaria

Jumanne Aprili 25 ni siku ya maadhimisho ya ungojwa wa malaria duniani, wakati ambapo katika nchi nyingi , hasa nchi za Afrika, changa moto bado ni kubwa katika kuutokomeza ugonjwa huo kama ambavyo malengo ya shirika la afya duniani WHO yalivyo ya kutokomeza ungojwa huo hadi ifikapo mwaka 2030.

Jamii ya mbu aambukizae ugonjwa wa Malaria.
Jamii ya mbu aambukizae ugonjwa wa Malaria. GETTY/DEA PICTURE LIBRARY
Matangazo ya kibiashara

Wakati dunia ikiadhimisha leo siku ya Malaria, Shirika la Afya Dunia, WHO, linasema chanjo ya kwanza ya malaria duniani itajaribiwa kwa kiwango kikubwa katika nchi ya Ghana, Kenya na Malawi kuanzia mwaka ujao.

Ripoti ya WHO kwa miaka miwili mfululizo 2015-2016 imebaini kwamba zaidi ya asilimia arobaini ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa malaria na pia kwa mujibu wa ripoti hiyo DRC na Nigeria zimekuwa nchi za kwanza duniani kuathiriwa na ugonjwa wa Malaria.

Shirika la Afya Duniani WHO limesema chanjo hizo zinaweza kuokoa maisha ya maelfu ya watu. Mpango huo ambao uko katika majaribio utahusisha zaidi ya watoto 700,000 wenye umri kati ya miezi mitano na mwaka mmoja na nusu.

Haijathibitika kwamba chanjo hiyo inaweza kufanya kazi kwa asilimia mia moja, lakini wataalamu wa masuala ya afya wanasema chanjo hiyo ni hatua muhimu katika mapambano ya dunia dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.