Wakaazi wa maeneo yalio karibu na Ziwa Oroville watakiwa kuhama
Watu zaidi ya 130,000 wanaoishi kaskazini mwa jimbo la California katika maeneo ambayo yaliyo karibu na bwawa refu zaidi nchini Marekani linalokabiliwa na hatari ya kubomaka wametakiwa kuhama mara moja.
Imechapishwa:
Mtaro wa uliodhoofishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika maeneo hayo huwa ukipitisha maji wakati wa dharura katika bwawa la Oroville. Maafisa wamesema wana hofu ya mtaro huo.
Ni mara ya kwanza kwa Ziwa Oroville kukumbwa na dharura ya aina hiyo katika miaka 50 tangu kujengwa kwa bwawa hilo.
Viwango vya maji katika bwawa hilo vimepanda zaidi kutokana na mvua kubwa pamoja na theluji, baada ya miaka mingi ya kiangazi mjini California.
Wataalam wamegundua kwamba baadhi ya vipande vikubwa vya saruji vilikuwa vimebambuka kutoka kwenye mtaro wa kuondosha maji kwenye bwawa hilo la Orovile.
Itafahamika kwamba hivi karibuni California ilikumbwa na majinga asili hasa majanga ya moto ambao uliteketeza baadhi ya kisitu na manyumba kadhaa na kusababisha maelfu ya watu kuyahama makaazi yao.