Pata taarifa kuu
CINA-MAZINGIRA

Beijing kupunguza matumizi yake ya makaa ya mawe mwaka huu

Beijing imepanga kupunguza kwa 30% mwaka huu matumizi yake ya makaa ya mawe, ili kuimarisha mapambano dhidi ya uchafuzi wa hewa, amesema Meya wa Beijing, Cai Qi, akinukuliwa na vyombo shirika la habari la Xinhua siku ya Jumapili.

Moshi mkubwa katika mji mkuu wa China, Beijing. Beijing inapanga kupunguza kwa 30% mwaka huu matumizi ya makaa ya mawe, ili kuimarisha mapambano dhidi ya uchafuzi wa hewa. Januari 26, 2017.
Moshi mkubwa katika mji mkuu wa China, Beijing. Beijing inapanga kupunguza kwa 30% mwaka huu matumizi ya makaa ya mawe, ili kuimarisha mapambano dhidi ya uchafuzi wa hewa. Januari 26, 2017. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Licha ya ahadi za mara kwa mara za hatua za kupunguza uchafuzi wa mazingira, sehemu kubwa ya kaskazini na kati ya China zimevamia tena katika msimu huu wa majira ya baridi na moshi mkubwa, ambao uvuruga safari za ndege, shughuli za bandari na shughuli katika mashule zilizorota.

"Tutajaribu kutumia mkaa wowote katika wilaya sita na sehemu za kusini ya Beijing mwaka huu," amesema Meya wa mji mkuu wa China.

"Tutapunguza matumizi ya makaa ya mawe kwa 30%, chini ya tani milioni saba mwaka 2017," Cai Qi ameendelea.

Beijing pia inaondoa barabarani mwaka huu magari 300,000 na kuendeleza mpango wa matumizi ya magari yanayotumia nishati ya "kijanir", shirika la habari la Xinhua limeandika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.