Pata taarifa kuu
GUINEA-AFYA-EBOLA

Guinea: Virusi vya Ebola mbioni kudhibitiwa

Majaribio ya chanjo cha ugonjwa wa Ebola yamebainika kuwa yana uwezo na nguvu zaidi dhidi ya virusi vya ugonjwa huo hatari, Wizara ya Afya ya Guinea imebaini baada ya kufanyiwa majaribio.

Timu kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu ikimsaafirisha mtu anayeshukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola, Januari 30, 2015 katika mji wa Forécariah, nchini Guinea.
Timu kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu ikimsaafirisha mtu anayeshukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola, Januari 30, 2015 katika mji wa Forécariah, nchini Guinea. REUTERS/Misha Hussain
Matangazo ya kibiashara

Majaribio hayo yamefanyiwa nchini Guinea,. Itakumbukwa kwamba Guinea ni moja ya nchi za magharibi ambazo zililikumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo hatari, na kusababisha vifo kadhaa.

Matokeo ya mwisho ya majaribio hayo, yalichapishwa kwenye jarida la maswala ya matibabu linalochapishwa nchini Uingereza, The Lancet.

Motokeo hayo yanaonyesha kuwa takriban watu 6,000 waliopata chanjo hiyo, walionekana hawana tena ugonjwa huo siku kumi baadaye, licha ya kuwa awali walikua waliambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola.

Mkurugenzi mkuu wa taasisi moja ya matibabu nchini Uingereza- Wellcome Trust, ameelezea matokeo hayo kama hatua chanya katika mapambano dhidio ya virusi hatari vya Ebola.

Itafahamika kwamba wanawake wengi wajawazito katika nchi hizo za Afrika magharibi walikua wakiogopa kwenda hospitali wakihofia kuambukizwa virisi vya ugonjwa huo hatari wa Ebola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.