Uingereza yaunga mkono mkataba kuhusu mabadiliko ya tabia nch
Uingereza imeridhia mkataba wa Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kujiunga na nchi nyingine zaidi ya 100 katika hatua ambayo wanaharakati wanasema wana matumaini kuwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump ataheshimu mpango huo.
Imechapishwa:
Wajumbe wanaohudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa wanaokutana tangu Jumatano wiki hii mjini Marrakech, nchini Morocco, wametoa wito kwa viongozi wa ngazi za juu wa kisiasa kuonesha dhamira ya dhati katika kupambana na suala hilo.
Wajumbe hao wanakutana huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kwamba rais mteule wa Marekani, Donald Trump, anaweza kujaribu kurudisha nyuma ahadi na jukumu la nchi yake ya kukataa gesi chafu.
Mkutano huo unatazamiwa kuhitimishwa eoIjumaa mjini Marrakech, nchini Morocco huku kukiwa na maazimio kadhaa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.