Pata taarifa kuu
DRC-AFYA

Chanjo ya homa ya manjano yaanza DRC

Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ushirikiano na Shirika la Afya duniani WHO inaanza leo Jumatano zoezi la kutoa chanjo ya homa ya manjano kwa raia wa nchi hiyo.

Mbu wa aina ya Aedes ambaye ni rahisi kuambukiza binadamu Homa ya manjano.
Mbu wa aina ya Aedes ambaye ni rahisi kuambukiza binadamu Homa ya manjano. ©Creative Commons
Matangazo ya kibiashara

Shirika la kihisani kutoka Uingereza la Save the Children linasema kwamba homa ya manjano nchini DRC na Angola inaweza hivi karibuni kuenea katika bara la Ulaya, Amerika na Asia. Ugonjwa wa homa ya manjano katika Afrika ni mbaya zaidi katika miaka hii 30 iliyopita.

Ripoti ya mwisho inabaini kwamba watu 400 walifariki katika nchi hizo mbili, ambapo wote wanashukiwa kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo.

Zaidi ya watu 6,000 wameambukizwa virusi vya homa ya manjano tangu kuzuka kwa ugonjwa huo, mwishoni mwa mwaka 2015 nchini Angola.

Hata hivyo, tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ghala za chanjo zitupu angalau mara nne.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limemelazimika kupunguza utaratibu wa vipimo ili kuweza kutoa chanjo kwa watu wengi zaidi.

Shirika lisilo la kiserikali kutoka Uingereza la Save the Children limetuma timu ya wataalam wa kusaidia Wizara ya Afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kampeni kabambe ya chanjo.

Shirika hili litaunga mkono juhudi za serikali ya Congo na kutoa chanjo kwa karibu watu 500,000 dhidi ya homa ya manjano katika maeneo ya mji wa Kinshasa.

Kampeni ya chanjo tayari iliendeshwa baada ya ugunduzi wa kuzuka kwa ugonjwa huo katika mji mkuu wa Congo, Kinshasa.

Wakati wa kampeni hii mpya ya chanjo, serikali ya Congo inapanga kutoa chanjo kwa watu milioni 10.5 dhidi ya homa ya manjano kati ya Agosti 17 na Agosti 26, 2016 katika kanda 48 za afya.

Serikali ya Congo imewatolea wito watu wote ambao ni walengwa na watoto wenye umri wa zaidi ya miezi 9 kwenda kwenye vituo maalumu kupata chanjo kwa bure.

Ugonjwa huu mara ya kwanza ulishuhudiwa nchini Angola, nchi jirani kabla ya kuenea nchini DRC.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema hakuna kesi mpya ambayo imeorodheshwa nchini Angola tangu mwezi Juni, hali ambayo inatoa matumaini kwamba ugonjwa huu sasa unaweza kuwa chini ya udhibiti nchini humo.

Homa ya manjano, ugonjwa ambao unaua, inaambukizwa na mbu walioambukizwa, hasa wa aina ya Aedes, walio katika nchi nyingi za Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.