Pata taarifa kuu
DRC-AFYA

Homa ya manjano yazuka DRC

Nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabilia na homa ya manjano baada ya tangazo rasmi la Waziri wa Afya Jumatatu hii asubuhi Juni 20.

Kampeni ya chanjo dhidi ya homa ya manjano. (Picha ya zamani).
Kampeni ya chanjo dhidi ya homa ya manjano. (Picha ya zamani). Claire Morin-Gibourg/RFI
Matangazo ya kibiashara

Mikoa mitatu, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Kinshasa tayari imekumbwa na janga hilo. serikali imesema watu 67 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya homa ya manjano, ikiwa ni pamoja na vifo vya watu watano.

Ili kukabiliana na hali hii ya dharura, serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Comno kupitia Waziri wake wa Afya, felix Kabange Numbi, imeomba msaada kwa Shirika la Afya Duniani pamoja na wafadhili wote kwa kuipatishia haraka chanjo.

Shirika la Afya Duniani katika taarifa yake ya hivi karibuni ilibaini kwamba idadi ya watu walioambukizwa virusi vya homa ya manjano imefikia 1,044 ikiwa ni pamoja na vifo 71 tangu mwezi Machi mwaka huu. Vipimo vinaendelea katika maabara. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mapambano dhidi ya janga hili katika mji kama Kinshasa ni changamoto kubwa. Changamoto ya vifaa ili kuwafikia wakazi zaidi ya milioni 10 wa mji mkuu, Kinshasa. Pia changamoto ya kupata chanjo kwa idadi ya kutosha. Chanjo ambayo inahitajika lakini haijapatikana. Homa ya manjano ilizuka nchini Angola mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.