Pata taarifa kuu
TANZANIA-AFYA

Zanzibar yakabiliwa na kipindupindu

Afisa wa afya Zanzibar anasema mlipuko wa kipindupindu katika kisiwa hicho umewaua watu wasiopungua 45 tangu mwezi Machi, kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press (AP).

Mji wa kitalii wa Zanzibar wa Stone.
Mji wa kitalii wa Zanzibar wa Stone. RFI
Matangazo ya kibiashara

Muhammed Dahoma, mkurugenzi wa Idara ya kuzuia na kudhibiti magonjwa katika wizara ya afya, alisema Jumatano kuwa watu 3,000 wamelazwa hospitalini kutokana na kipindupindu.

Serikali ya Zanzibar hivi karibuni imechukuliwa hatua za kuondokana na kuzuka kwa ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku uuzaji wa chakula na juisi katika maeneo ya wazi. Serikali pia imeanzisha kambi kadhaa katika visiwa vya Unguja na Pemba ambapo wagonjwa wa kipindupindu wametengwa sehemu.

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya Zanzibar, zimeziba mifereji ya maji taka na kuzidisha matatizo ya kipindupindu.

Mlipuko wa kipindupindu unatishia kuiathiri sekta ya utalii katika kisiwa cha Zanzibar, hasa kama utaendelea hadi mwezi Juni wakati ambapo watalii wengi wanakua wameingia katika kisiwa hicho kuzuru maeneo mbalimbali ya kitalii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.