Pata taarifa kuu
MALARIA-AFYA

Madagascar: watu 740,000 wakabiliwa na Malaria

Katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa dhidi ya Malaria Aprili 25, Madagascar imesema kuwa inaendelea kushuhudia ongezeko la ugonjwa wa Malaria.

Chandarua ni njia bora zaidi ya kuzuia Malaria.
Chandarua ni njia bora zaidi ya kuzuia Malaria. © AFP/ALEXANDER JOE
Matangazo ya kibiashara

Raia wa Madagascar hawajiepushi na ugonjwa huo. Mwaka jana karibu watu 570 walipoteza maisha kutokana na Malaria na watu 740 000 waliumwa katika eneo la Grande Ile.

Lengo la Serikali ya Madagascar liko wazi: kupunguza nusu ya idadi ya wagonjwa wa malaria katika mwaka 2017. Kwa kufanikisha hilo, juhudi zimefanywa ikiwa ni pamoja na usambazaji bure wa vyandarua milioni 10 vyenye dawa mwaka 2015. Kampeni za uhamasishwaji kwa wakuu wa wilaya na kata na kwa walimu wa shule ziliendeshwa.

Vipimo vya uchunguzi vya haraka na vya bure pia vimeongezeka: vipimo milioni 1.5 mwaka jana dhidi 600,000 mwaka 2010. Pamoja na jitihada hizi, malaria iliua karibu watu 570 mwaka 2015.

Tatizo la kwanza: kutengwa kwa wakulima wengi ambao wanaishi mbali zaidi kutoka vituo vya afya vya mwanzo. Vile vile, kwa manyasi makubwa, wachimba migodi wakati mwingine wanatembea kwa siku kadhaa kwa kutafuta dhahabu na wala hawabebi dawa za kutumia kwa wagonjwa wa Malaria.

Sababu ya pili inayoongeza malaria: vimbunga na mafuriko ya mara kwa mara vimemeharibiwa nyumba nyingi na kusababisha kuenea kwa mbu.

Hatimaye, baadhi raia wa Madagascar wamekua wakitumia imani za kishirikina au hirizi badala ya kutafuta matibabu hospitalini. Changamoto nyingine kwa serikali ni kuongeza uhamasishwaji kwa kuondoa moja kwa moja au kufunika mifereji na visima ambavyo ni sehemu wanapozalia m'bu.

Duniani kote, Malaria imeua zaidi ya watu 430,000 mwaka jana, wengi wao wakiwa barani Afrika hasa katika Ukanda wa Sahara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.