Pata taarifa kuu
MISRI-MOBARAK-SIASA

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak afariki dunia

Hosni Mubarak amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91 katika hospitali ya jeshi ya Galaa huko Cairo, Jumanne hii Februari 25, 2020. Mkwewe, Jenerali Mounir Thabet, ndiye ametangaza kifo chake.

Rais wa Misri Hosni Mubarak huko Cairo, Desemba 11, 2010.
Rais wa Misri Hosni Mubarak huko Cairo, Desemba 11, 2010. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Hosni Mubarak alitawala Misiri kwa mkono wa chuma kwa kipindi cha miaka 30, hadi alipong'atuliwa mamlakani kufuatia maandamano makubwa ya umma mnamo mwaka 2011.

Rais wa sasa wa Misri, Abdel Fattah Al Sisi, ambae ikulu ilituma rambirambi za pole kwa familia ya Mubarak, imemuelezea kuwa miongoni mwa ''mashujaa wa vita vya oktoba 73'' dhidi ya Israel, vita ambavyo Hosni Mubarak aliongoza kikosi cha jeshi la anga.

Hosni Mubarak aliendelea kuchukua jukumu muhimu katika vita kati ya Israel na Waarabu 1973.

Alikuwa rais chini ya muongo mmoja baadaye, kufuatia, mauaji ya rais Anwar Sadat.

Alikuwa na jukumu muhimu katika mchakato wa amani wa Israel - Palestina.

Hosni Mubarak alizaliwa Mei 4, 1928 katika eneo la Nile Delta. Mara tu alipomaliza shule ya upili, alijiunga na Chuo cha kijeshi cha Misri, kisha mwaka 1950 Chuo cha jeshi la wanaanga ambapo alimaliza masomo yake makuu akiwa na cheo cha meja.

Mubarak alidumu madarakani kwa miongo mitatu kabla ya kung'atuliwa jeshi baada ya maandamano makubwa ya raia.

Alikutwa na hatia ya kula njama katika mauaji ya waandamanaji wakati wa mapinduzi na kuwekwa kizuizini.

Alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha jela mnamo mwaka 2012 kwa madai ya kula njama ya mauaji ya waandamanaji 239, lakini mahakama ya rufaa iliamuru kesi hiyo kusikilizwa upya na hatimaye mashitaka yake yalifutwa na aliachiliwa mwaka 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.