Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-MANDELA-SIASA-USALAMA

Afrika Kusini yadhimisha miaka 30 tangu Nelson Mandela aachiwe huru

Miaka thelathini imekamilika leo tangu mtetezi wa wanyonge Nelson Mandila Madiba, rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini kuachiliwa huru, baada ya kuzuiliwa kwa kipindi cha miaka 27 wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi (Apartheid) nchini humo.

Nelson Mandela na mkewe Winnie.
Nelson Mandela na mkewe Winnie. Trevor SAMSON/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mandela aliachiliwa huru kutoka gerezani Februari 11, 1990, katika hatua ya kihistoria ya safari ya Afrika Kusini kuelekea kwenye demokrasia, ambayo ilitimizwa miaka minne baadaye.

Akizungumza siku moja kabla ya nchi hiyo kuadhimisha miaka 30 tangu Nelson Mandela aachiliwe huru, rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema ukosefu wa usawa, ajira, umasikini na vurugu vimeendelea kuwa changamoto kubwa kwa nchi hiyo, miaka 30 baada ya Mandela kuachiwa huru.

Rais Ramaphosa amewataka raia wa nchi hiyo kuwa na umoja katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili Afrika Kusini kwa sasa;

Wadadisi wanasema baada ya Nelson Mandela kuachiliwa huru, Afrika Kusini ilibadilika, si tu kwa raia wa nchi hiyo, lakini kwa Waafrika wengine waliohamia nchini humo kwa matumaini ya kupata maisha bora.

Kwa dunia nzima Mandela alikua ishara ya mambo mengi, sio kiongozi tu lakini mfano wa viongozi ambao dunia insatahili kua nao enzi hizo.

Wengi wanamfahamu Mandela kwa kua na moyo mwepesi wa kusamehe na wengi wanamkumbuka hivyo kwani baadhi walimshangaa sana miaka ya tisini, aliposema kuwa hana chuki na mtu na kuwa amewasamehe waliomtendea ubaya na hata kumfunga. Hakuwa na uchungu wowote na FW De Klerk.

Msimamo wake ulijulikana na kufafanuliwa vyema katika kesi iliyohujumiwa mwaka 1964. Alisema, ‘Nimepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi na pia nimepigana dhidi ya utawala wa waaafrika weusi usiofaa.’’

"Nimekuwa nikiota kuhusu jamii huru, ambapo kila mtu ataishi na jirani yake bila uhasama, wala chuki na kuwa na fursa nzuri. Lakini pia ikiwa itahitajika, ninaweza kutoa uhai wangu kwa ajili ya vita kama hivi."

Alizaliwa mwaka 1918,katika Rolihlahla Dalibhunga, na kulelewa katika kijiji cha Mvezo Mashariki mwa mkoa wa Cape. Alikuwa na ndugu zake 13 katika familia iliyokuwa na uhusiano wa karibu na familia ya kifalme ya Thembu.

Nelson Mandela alienziwa na wengi kwa sababu ya vita alivyopigana dhidi ya utawala wa wazungu

Babake alifariki Mandela akiwa na umri wa miaka tisa. Alimtaja babake kama mtu mkali mwenye kutaka watu kufuata maadili mema.

Nelson Mandela alisomea katika shule ya kimethodisti, na kisha mwaka 1939 akaenda katika chuo kikuu cha Fort Hare .

Mandela alikutana na Oliver Tambo,ambaye alianzisha naye kampuni ya sheria ya kwanza kumilikiwa na Waafrika weusi nchini humo.

Wote wawili walifukuzwa kutoka chuoni kwa sababu za kisiasa.

Mwanzo alikua wakili kisha mwanaharakati na kisha akaanza vita dhidi ya utawala wa Wazungu.

Miaka ya hamsini na mapema miaka ya tisini, wakati maandamano yao yalipotibuliwa kwa nguvu, chama cha ANC kikaanza vita halisi dhidi ya utawala wa wazungu.

Alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la uhaini mwaka 1956.

Baada ya kesi yake kudumu miaka mitano, aliachiliwa huru.

Lakini ANC kikawa kimepigwa marufuku, naye Oliver Tambo akatoroka nchi hiyo.

Mandela naye pia alijificha na kuendeleza harakati zake kichini chini na kuanza safari zake nje ya nchi kutaka usaidizi kwa mataifa mengine. Pia alimtembelea Tambo mjini London.

Lakini aliporejea ndipo sasa akakamatwa na kufungwa maisha jela, kwa miaka 27 kwa madai ya kuhujumu serikali.

Alifanya kazi katika machimbo ya mawe akiwa gerezani katika kisiwa cha Roben. Daima alisema gerezani alikua na muda mwingi wa kutafakari maisha.

Baada ya kuondoka jela mwishoni mwa kifungo chake cha miaka 27, maisha ya Mandela yalikuwa yamekomaa, na ilikua dhahiri kua walimnyang’anya Mandela ujana wake.

Ndoa yake kwa Winnie Mandela ilimalizika baada ya wawili hao kuachana. Marafiki zake wakawa hawapo tena.

Lakini alipokewa vyema sana na umati mkubwa wa watu alipoondoka gerezani.

Katika hali hiyo, angekuwa kiongozi mwingine, angemlaumu adui wake lakini Mandela pia aliwalaumu waafrika wenzake hasa wa chama cha ANC aliosema wanawaua watu na kua waache tabia hiyo.

Alijua watu wasingependa ujumbe wake, lakini pia alijua hawatamsikiliza.

Chama cha ANC kilishinda kwani watu wengi walikuwa na imani nacho.

Mfahamu Madiba Nelson Mandela

Nelson Mandela Februari 25, 1990, siku chache baada ya kuachiliwa huru.
Nelson Mandela Februari 25, 1990, siku chache baada ya kuachiliwa huru. Trevor Samson/AFP

1918 Alizaliwa katika mkoa wa Eastern Cape

1943 Akajiunga na chama cha ANC

1956 Alifunguliwa kesi ya uhaini lakini baada ya miaka mine kiasi ikatupiliwa mbali

1962 Alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la uchochezi na kufungwa jela miaka mitano

1964 Alishitakiwa kwa kosa la kuhujumu serikali na kufungwa maisha jela

1990 Aliachiliwa kutoka gerezani

1993 Ashinda tuzo ya Amani ya Nobel

1994 Alichaguliwa Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini

1999 Ang’atuka mamlakani

2001 Aligunduliwa kua na Saratani ya tezi kibofu

2004 Alistaafu

2005 Alitangaza kua mwanawe alifariki kutokana na maradhi ya Ukimwi

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.