Pata taarifa kuu
LIBYA-UN-ANTONIO-USALAMA-SIASA

Antonio Guterres: Nina "matumaini" ya mapigano kusitishwa haraka huko Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa Antonio Guterres amesema kuna matumaini ya kupatikana kwa makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano nchini Libya, nchi ambayo inaendelea kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Februari 9, 2020, wakati wa mahojiano na RFI na France 24.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Februari 9, 2020, wakati wa mahojiano na RFI na France 24. RFI-France 24
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kinachokwamisha kufikia makubaliano ya kudumu ni uingiliaji wa mataifa ya kigeni katika mzozo wa Libya.

Akihojiwa jana jijini Addis Abeba katika mahojiano maalum ya RFI na France 24, Guterres amesema pande zote mbili zimekubaliana kwa lengo matatu muhimu, lakini kubwa zadi ni makubaliano ya kusitishwa vita kuwa ya kudumu.

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umependekeza duru mpya ya mazungumzo kati ya pande mbili zinazohasimiana nchini Libya ifanyike mjini Geneva wiki ijayo, baada ya mazungumzo mengine yaliofanyika hivi karibuni kumalizika bila ya maafikiano yoyote ya kumaliza mgogoro huo.

Kamisheni ya pamoja ya kijeshi inayojumuisha maafisa watano kutoka pande zote mbili ilikuwa ikikutana mjini Geneva kuanzia tarehe 3 Februari hadi Jumamosi wiki iliyopita.

Pande hasimu zimekubali kukaa tena katika meza ya mazungumzo, kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo. Umoja wa Mataifa umependekeza mkutano huo kufanyika tarehe 18 mwezi huu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.