Pata taarifa kuu
RWANDA-EAC

Rwanda kuwafunza wafanyabiashara wake Kiswahili

Katika harakati za kuwasaidia wafanyabiashara wa Rwanda wanaokumbana na changamoto ya mawasilano pale wanapokwenda nchi jirani zinazotumia lugha ya Kiswahili, nchi ya Rwanda kwa ushirikiano na kamisheni ya kiswahili ya Jumuhiya ya Afrika Mashariki inaanda mafunzo ya Kiswahili yatakayotolewa kwa wafanyabiashara hao.

Soko la matunda la Kigali, Rwanda.
Soko la matunda la Kigali, Rwanda. RFI/Laure Broulard
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya utafikiti uliofanywa na kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye nchi wanachama kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili, huku baadhi ya wafanyabiashara wakizungumzia changamoto wanazokutana nazo wanapokua nchi jirani zinazozungumza Kiswahili.

Claire Butoyi ni mfanyabiashara wa nguo soko kuu la Kigali, anaseme “Wafanyabiashara wa Rwanda wanapata changamoto wanapokua nchi zinazozungumza kiswahili ,inapidi watumie watu wa kulipia wakuwasaida wanapokua sokoni na wakati mwingine wanapandishiwa bei ,wangekua wanajua kiswahili hayo hayangetokea”.

Profesa Simala Keneth ni katibu mtendaji wa kamisheni ya Kiswahili amesema lugha ya Kiswahili ni moja ya chombo kinachoweza kuchangia katika kuinua uchumi wa nchi wanachama kikitumiwa kama lugha ya mawasiliano.

Jumuhiya ya Afrika mashariki iliandaa mkutano mkubwa wa wafanyabiasharabhapa mjini Kigali kilichodhihilika ni kwamba wafanyabiashara wa nchi moja hawangeweza kuwasiliana na wafanyabiashara wa nchi nyingine na hii ilitokana na kwamba hakikuwa na lugha moja ingewasidia kuwasiliana”, alisema profesa Kenneth.

Wadau wa Kiswahili nao wamezungumzia hatua hii ya utoaji wa mafunzo kwa wafanyabiashara wa Rwanda, Isidori GAHAMANYI ni mdau wa Kiswahili, anasema “Itasaidia kufungua mlango ,wafanyabiashara wa Rwanda wanayoa bidhaa kwenye bandari za Mombasa na Daresalaam ,na raia wa kule wanazungumza kiswahili , nadhani wanyarwanda watafaidika sana”.

Soko la biashara kwenye jumuhiya ya afrika mashariki ni moja ya fursa inayotumiwa katika kuinua uchumi, Kiswahili hutumiwa kama chombo cha mawasiliano.

Rwanda iliidhinisha Kiswahili kua lugha rasmi nchini humo mwaka 2017.

Ripoti hii ni ya mwandishi wetu wa Kigali, Edith Nibakwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.