Pata taarifa kuu
MALAWI-SIASA-USALAMA-HAKI

Kesi ya kupinga ushindi wa Mutharika: Hali ya wasiwasi yatanda Malawi, shule zafungwa

Wananchi wa Malawi leo Jumatatu wanasubiri uamuzi wa Mahakama, kuhusu kesi ya kupinga ushindi wa rais Peter Mutharika, kufuatia Uchaguzi Mkuu uliyofanyika mwaka uliopita.

Mahakama ya nchini Malawi iliitaka Tume ya Uchaguzi (MEC) isitishe kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Mei 21 kwa sababu ya madai ya udanganyifu.
Mahakama ya nchini Malawi iliitaka Tume ya Uchaguzi (MEC) isitishe kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Mei 21 kwa sababu ya madai ya udanganyifu. AMOS GUMULIRA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kuna hali ya wasiwasi hasa katika jiji kuu la Lilongwe, huku shule zikifungwa lakini pia idadi ya watu wameamua kusalia nyumbani kwa kuhofia machafuko baada ya uamuzi huo.

Mwanasiasa wa upinzani Lazarus Chakwera alikwenda Mahakamani kupinga ushindi wa rais Mutharika, katika uchaguzi ambao ulikuwa na ushindani mkali, akidai aliibiwa kura.

Licha ya serkali kutoa wito wa amani, wakuu wa Shule nchini humo wanasema wamefikiana uamuzi wa kufunga shule kwa hofu kuwa huenda ghasia zikashuhudiwa baada ya uamuzi huo.

Rais wa Malawi Peter Mutharika alichukua uongozi wa asilimi 40.44 ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei huku ikiwa asilimia 75 ya kura hizo zilihesabiwa kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.

Lazarus Chakwera , ambaye anaongoza chama pinzani cha Malawi Congress Party, alijipatia asilimia 35.34, huku makamu wa rais Saulos Chilima akipata asilimia 18.35, tume hiyo ilisema katika mkutano na waandishi wa habari.

Uchaguzi huo ulikumbwa na ushindani wa karibu kati ya rais Peter Mutharika, makamu wake Saulos Chilima na Chakwera ambaye anakiongoza chama cha Malawi Congress party.

Katika uchaguzi wa 2014 , Chakwera alipoteza kwa karibu dhidi ya rais Mutharika na akashindwa kupinga uchaguzi huo mahakamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.