Pata taarifa kuu
UFARANSA-SAHEL-USALAMA-WANAJESHI

Ufaransa kutuma wanajeshi wengine 600 katika eneo la Sahel kupambana na ugaidi

Ufaransa imetagaza kutuma wanajeshi wake zaidi eneo Sahel barani Afrika, kwa kutuma wanajeshi wengine 600, kuungana na 4,500 ambao wameendelea kupambana na makundi  ya kijihadi katika eneo hilo.

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Florence Parly
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Florence Parly Zach Gibson / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi Florence Parly, amesema wanajeshi  hao watawasili katika nchi hizo za Sahel za Mali, Burkina Faso na Nigermwisho wa mwezi wa pili, ili kuungana na wenzao kuendeleza operesheni hiyo.

Hata hivyo, Ufarabsa imetoa wito wa nchi za Sahel kuonesha juhudi katika vita hivyo vya kigaidi, baada ya Paris kupoteza wanajeshi wake 13 baada ya kuangushwa kwa ndege yao kimakosa mwezi Novemba mwaka 2019.

Ajali hiyo, ilikuwa mbaya zaidi kuwahi kulikumbuka jeshi la Ufaransa kwa muda mrefu huku rais Emmanuel Macron akisema serikali yake itafanya uamuzi kuhusu kuendelea kuwepo kwa vikosi vyake katika eneo hilo.

Kabla ya hatua hii, rais Macron hivi karibuni akikutana na viongozi wa eneo la Sahel jijini Paris aliahidi kutuma wanajeshi 220 katika eneo hilo ambalo pia linajumuisha mataifa ya Chad na Mauritania.

Chad nayo imesema itaongeza kikosi chake katika jeshi la G 5 Sahel, huku Jamhuri ya Czech nayo ikiahidi kutuma wanajeshi  wake 60.

Wachanmbuzi wa masuala ya usalama, wanaoanagzia vita dhidi ya ugaidi katika eneo la Sahel, wanasema  hatua hii ya Ufaransa imekuja, baada ya Marekani kusema kuwa inapanga kupunguza wanajeshi wake barani Afrika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.