Pata taarifa kuu
DRC-UN-HAKI ZA BINADAMU

UN: Ukiukaji wa haki za binadamu wapungua kidogo DRC

Idadi ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepungua kidogo tangu kuingia madarakani Félix Tshisekedi.

Askari polisi huko Kinshasa.
Askari polisi huko Kinshasa. REUTERS/Robert Carrubba
Matangazo ya kibiashara

Visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini DRC vimepungua kwa asilimia nne tu, ofisi ya mseto ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema. Katika ripoti yake ya kila mwaka, UNJHRO inasema kwamba maafisa wa serikali ni wahusika wakuu wa vitendo hivyo.

Mwaka wa 2019, maafisa wa serikali waliendelea kuhusika kwa asilimia 54 katika vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyotekelewza kote nchini. Mwaka 2018, mwaka mmoja kabla ya muhula wa mwisho wa Joseph Kabila kutamatika, ilikuwa ni 61%.

Ikumbukwe kwamba maafisa wakuu wa idara za usalama hawakubadilishwa katika utawala huu wa Félix Tshisekedi. Mwaka huu tena, vikosi vya jeshi na polisi vimeendelea kunyooshewa kidole na ofisi ya msteo ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Vikosi hivyo vimehusika katika mateso na mauaji ya ya kiholela. Katika maeneo ya migogoro, jeshi la DRC, FARDC, limekuwa likihusika na vitendo vya ukiukaji mkubwa kuliko kundi lolote la watu wenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.