Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MISRI-SUDAN-NILE-USHIRIKIANO

Mkataba kuhusu matumizi ya Mto Nile mashakani

Siku ya mwisho ya kupata mwafaka kuhusu mzozo wa matumizi ya Mto Nile kati ya Misri na Ethiopia, imepita bila ya kusikia lolote kutoka kwa pande zote zinazokinzana au wasuluhishi wa mzozo huu.

Bwawa lililojengwa kwenye Mto Nile Ethiopia, Septemba 26, 2019.
Bwawa lililojengwa kwenye Mto Nile Ethiopia, Septemba 26, 2019. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa mambo ya nje pamoja na wale wa maji kutoka mataifa hayo mawili, wakiwemo wale kutoka Sudan kwa siku mbili zilizoopita, wamekuwa wakikutana jijini Washington DC nchini Marekani kupata suluhu ya mzozo huu ambao ulianza kushuhudiwa baada ya Ethiopia kuamua kutumia bwawa la kuzalisha umeme kutumia maji hayo.

Tarehe 15 mwezi huu wa Januari, Marekani ikishirikiana na Benki ya dunia, ilitangaza kuelekea kupata suluhu, lakini haikufamika makubaliano hayo yaatanza kutekelezwa lini.

Mzozo huu kati ya Ethiopia na Misri, umekuwa ukiendelea kwa miaka kadhaa sasa, huku Ethipia ikisema ina haki za kutumia maji hayo kwa ajili ya mradi wake wa umeme, lakini Misri inasema hatua hiyo sio ni uonevu kwa wananchi wake kwa sababu inategemea maji ya mto nile kwa asilimia 90 katika shughuli zote.

Ethiopia inasema haiwezi kusitisha mradi huo wa Dola Bilioni 4 ambao ulianza mwaka 2011, kwa sababu inasambaza asilimia 85 ya maji ya mto Nile.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.