Pata taarifa kuu
MALAWI-SIASA-USALAMA-HAKI

Hali ya wasiwasi yatanda Malawi

Shule za mabweni nchini Malawi zinafungwa kuelekea wiki ijayo, wakati Mahakama itakapotoa uamuzi wa kesi ya kupinga ushindi wa rais Peter Mutharika.

Peter Mutharika akizindua kampeni yake ya uchaguzi Aprili 7, 2019.
Peter Mutharika akizindua kampeni yake ya uchaguzi Aprili 7, 2019. AMOS GUMULIRA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hali ya wasiwas inashuhudiwa nchini humo kuelekea siku ya Jumatatu wakati uamuzi huo utakapitolewa na hii ilikuja baada ya Lazarus Chakwera aliyekuwa mpinzani wa karibu wa rais Mutharika kudai wizi wa kura katika uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali.

Licha ya serkali kutoa wito wa amani, wakuu wa Shule nchini humo wanasema wamefikiana uamuzi wa kufunga shule kwa hofu kuwa huenda ghasia zikashuhudiwa baada ya uamuzi huo.

Rais wa Malawi Peter Mutharika amechukua uongozi wa asilimi 40.44 ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei huku ikiwa asilimia 75 ya kura hizo zimehesabiwa kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.

Lazarus Chakwera , ambaye anaongoza chama pinzani cha Malawi Congress Party amejipatia asilimia 35.34 huku makamu wa rais Saulos Chilima amejipatia asilimia 18.35, tume hiyo iliambia mkutano na wanahabari.

Uchaguzi huo ulikumbwa na ushindani wa karibu kati ya rais Peter Mutharika, makamu wake Saulos Chilima na Chakwera ambaye anakiongoza chama cha Malawi Congress party.

Katika uchaguzi wa 2014 , Chakwera alipoteza kwa karibu dhidi ya rais Mutharika na akashindwa kupinga uchaguzi huo mahakamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.