Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SORO-SIASA-USALAMA

Soro kuwania uchaguzi wa urais licha ya waranti wa kukamatwa

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Cote d'Ivoire Guillaume Kigbafori Soro anaendelea na msimamo wake wa kuwania katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 31 licha ya waranti wa kukamatwa uliyotolewa dhidi yake na mahakama ya Cote d'Ivoire, kwa mujibu wa shirika la Habari la Reuters.

Guillaume Soro, kiongozi wa zamani wa waasi na waziri mkuu wa zamani wa Cote d'IvoireFebruari 8, 2019.
Guillaume Soro, kiongozi wa zamani wa waasi na waziri mkuu wa zamani wa Cote d'IvoireFebruari 8, 2019. EUTERS/Thierry Gouegnon/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa urais nchini Cote d'Ivoire umepangwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.

Kiongozi wa zamani wa waasi na waziri mkuu wa zamani, anayeshtumiwa kutaka kufanya mapinduzi na ambaye anakabiliwa na kifungo cha maisha, anatafutwa na waranti wa kukamatwa iliyotolewa usiku wa mkesha wa Krismasi wakati alikuwa katika hatua ya kurejea nchini Cote d'Ivoire. Hata hivyo Guillaume Soro amekanusha mashtaka dhidi yake.

"Mimi ni mgombea katika uchaguzi wa urais katika nchi yangu Cote d'Ivoire Oktoba 31. Nataka kuwaambia hilo, ninabaki na nia yangu hiyo. Wale ambao walinizuia kuingia katika nchi yangu Desemba 23 mwaka jana hawatanizuia kamwe kuwania katika uchaguzi wa urais, "amesema katika mahojiano, na kuongeza kuwa" hatoachana na mpango huo hata kama atafanyiwa madhila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.