Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MDC-SIASA-UCHUMI

Chamisa: Tunapaswa kufanya maandamano kushinikiza mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi Zimbabwe

Kiongozi mkuu wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa ametangaza maandamano zaidi anayosema, yanalenga kushinikiza mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini humo.

Kiongozi wa upinzaji nchini Zimbabwe Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari.
Kiongozi wa upinzaji nchini Zimbabwe Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Chamisa amesema maandamano hayo yanayoandaliwa na chama chake cha MDC, ndio njia pekee ya raia wa nchi hiyo kufikia malengo yao, na kuwaondoa katika mateso wanayopitia nchini ya rais Emmerson Mnanganagwa.

Tangu alipoingia madarakani, uongozi wa rais Mnangangwa umeendelea kukabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na kisiasa, wakati huu mataifa ya Magharibi yakiendelea kuiwekea vikwazo vya kiuchumi taifa hilo la Kusini mwa bara la Afrika.

Wazimbabwe wengi wanaonekana kuwa katika hali mbaya zaidi leo kuliko hapo mwaka 2009, pale taifa hilo la kusini mwa Afrika lilipoachia sarafu yake isiyo na thamani na kuanza kutumia sarafu mbali mbali hususan dola ya marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.