Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

DRC: Félix Tshisekedi aonya washirika wake wa FCC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi ametishia kuwafuta kazi Mawaziri wake na hata kulivunja bunge, iwapo washirika wake wa kisiasa ambao wanaegemea katika mrengo wa rais wa zamani Joseph Kabila, wataendelea kumdharau.

Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, Novemba 9, 2019.
Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, Novemba 9, 2019. © Sumy Sadurni / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi amesema kuna baadhi ya Mawaziri ambao wamekuwa wakimwambia kuwa, wanapata shinikizo, na kusisitiza kuwa, hana nioa ya kulivunja bunge lakini, iwapo mzozo utazuka, atalazimika kufanya hivyo.

"Ni kweli kwamba miongoni mwa wananchi wenzetu, wote sio wenye nia nzuri. Katika muungano wetu, sio kila mtu amejumuishwa kwa ushindi wa raia. Niko madarakani kwa mapenzi ya raia na ya Mungu, sio kwa mapenzi ya mtu. Majukumu yangu ni kuwatumikia raia wangu. Yeyote anayepinga, hasa ikiwa ni waziri aliyeteuliwa na mimi, atachukuliwa hatua. Kila siku ninapoongoza Baraza la Mawaziri, ninawakumbusha maadui wa FCC kuwa najua walitia saini kwenye hati. Kufikia sasa, sijaona waziri yeyote akipinga maamuzi yangu. Lakini baadhi ya mawaziri wananiambia kwamba wanapata shinikizo. Baadhi yetu, wanatuomba tusifanye kazi kama inavyotakiwa, walesema mawaziri hao. Raia wa DRC wameniamini wakanipa majukumu, nakuwajibika kwa hilo. Na yeyote ambaye hataki kufuata maagizo yangu na ambaye atashikamana na maagizo ya chama chake cha siasa, atafukuzwa, " ameonya rais Félix Tshisekedi.

Rais Tshisekedi amabye amekuwa madarakani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, aliingia katika maelewano na chama cha zamani cha rais Joseph Kabila Kqbqnge cha PPRD, kushirikliana naye katika serikali yake, baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.