Pata taarifa kuu
AFRIKA-MJANGA ASILI-NJAA

UN: Watu milioni 45 wakabiliwa na kitisho cha njaa kusini mwa Afrika

Umoja wa Mataifa umeonya kwamba watu milioni 45 wanakabiliwa na kitisho cha njaa kusini mwa Afrika kwa sababu ya ukame, mafuriko na hali mbaya ya uchumi katika nchi za ukanda huo.

Ukame mkubwa na joto kali vimeharibu mazao ya mahindi nchini Zimbabwe.
Ukame mkubwa na joto kali vimeharibu mazao ya mahindi nchini Zimbabwe. ALEXANDER JOE / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kitisho hiki cha njaa kimefikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa na kuna hatari hali hii izidi kuwa mbaya," mkuu wa shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Kusini mwa Afrika , Lola Castro ameonya.

Kwa miaka mitano, maeneo ya Kusini mwa bara la Afrika yamekumbwa na upungufu mkubwa wa mvua, hali inayosababishwa na kurejea kwa mara kwa mara kwa kipindi cha mvua za El Nino El Nino, zinazoharibu mazao ya kilimo ya nchi hizo kumi na sita, ambazo, nyingi ni maskini zaidi duniani.

Joto kali ulimwenguni pia husababisha vimbunga vikali.

Mwaka jana kimbunga Idai kilisababisha mafuriko mabaya katika nchi za Msumbiji, Zimbabwe na Malawi, na kusababisha watu wengi kupoteza maisha, na kuwaacha mamilioni ya watu bila makaazi na mali zao kuharibiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.