Pata taarifa kuu
LIBYA-UTURUKI-USALAMA

Erdogan aanza kupeleka wanajeshi Libya

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangaza Alhamisi wiki hii kwamba anaanza kupeleka wanajeshi nchini Libya kusaidia vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa ya Fayez al Sarraj dhidi ya vikosi vya Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita mashariki mwa Libya.

Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj akizuru ngome iliyowekwa chini ya himaya ya jeshi la serikali ya Tripoli kutoka mikononi mwa vikosi vya Marshal Haftar, magharibi mwa Tripoli, Aprili 5, 2019.
Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj akizuru ngome iliyowekwa chini ya himaya ya jeshi la serikali ya Tripoli kutoka mikononi mwa vikosi vya Marshal Haftar, magharibi mwa Tripoli, Aprili 5, 2019. REUTERS/Hani Amara
Matangazo ya kibiashara

Wiki mbili zilizopita Bunge la Uturuki lilipitisha uamuzi unaomruhusu rais Recep Tayyip Erdogan kuanza kupeleka vikosi vya nchi hiyo nchini Libya.

Tangazo la kupeleka wanajeshi wa Uturuki linakuja siku tatu kabla ya mkutano wa kimataifa kuhusu mgogoro wa Libya utakaofanyika jijini Berlin, nchini Ujerumani.

Rais wa Uturuki atashiriki mkutano huo, baada ya kushindikana kwa mazungumzo mapema wiki hii jijini Moscow kati ya mahasimu wawili nchini Libya, ambapo Khalifa Haftar amekataa kutia saini makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa chini ya upatanishi wa Uturuki na Urusi.

Erdogan ameongeza kuwa Uturuki itaendelea kutumia njia zake zote za kidiplomasia na kijeshi kuhakikisha utulivu katika mpaka wake wa kusini, ardhini au baharini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.