Milio ya risasi yasikika katika kambi mbili za idara za usalama Khartoum
Miezi mitano baada ya serikali ya raia nchini Sudani kuundwa, milio ya risasi imesikika katika kambi mbili za idara za usalama jijini Khartoum. Hali ambayo imezua wasiwasi mkubwa miongoni mwa wakaazi wa mji huo. tukio lililotokea Jumatatu mchana Januari 14.
Imechapishwa:
Kwa mujibu wa ikulu ya rais, hali hiyo imetokea katika moja ya kitengo cha idara ya ujasusi, ambacho kinatarajiwa kuvunjwa, ambapo baadhi ya maafisa wa usalama wenye hasira walijaribu kuandamana.
Tukio hilo lilizua wasiwasi mkubwa katika mji wa Khartoum. Milio mingi ya ya risasi ilisikika Januari 14, huku barabara zikifungwa, wanajeshi wengi walitumwa katika maeneo mbalimbali ya mji na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum ulifungwa kwa muda wa saa chache.
Ikulu ya rais imebaini kwamba hali hiyo imezushwa na askari waliokataa kulipwa fidia waliyopewa wakati wa kustaafu kwao na kwamba mazungumzo yanaendelea.
Inaonekana makabiliano yalitokea kati ya vikosi vya serikali, jeshi au Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) na idaya ya ujasusi (NISS). Mkuu wa kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) anamtuhumu Salah Gosh, mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi (NISS) na moja wa vigogo katika utawala wa Omar al-Bashir, kuwa anahusika katika mstari wa mbele na hali hiyo.
Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Waziri Mkuu Abdalla Hamdok amewahakikishia raia kwamba kila kitu kiko chini ya udhibiti na kwamba vikosi vya jeshi vya Sudan vina uwezo wa kushughulikia hali hiyo.
We want to assure the Sudanese people that the incidents which took place today are under control and they will not stop us and our mission nor will they be a reason for us to retreat from the goals of this revolution. pic.twitter.com/jQ4qduRrc1
Abdalla Hamdok (@SudanPMHamdok) January 14, 2020