Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Kumi na nane wauawa karibu na mgodi wa dhahabu wa Salamabila, DRC

media Jeshi al DRC laendelea kukabiliana na makundi yenye silaha, haswa Mashariki mwa nchi hiyo, katika mikoa ya Maniema, Kivu Kusini na Kaskazini. ALEXIS HUGUET / AFP

Watu kumi na wanane, wakiwemo watoto wameuawa baada ta mapigano kuzuka kati ya jeshi na kundi la waasi katika eneo la mgodi unaowaniwa katika eneo la Salamabila , Mashariki mwa nchi hiyo.

Maafisa wanasema, watu waliouwa walipigwa risasi na wengine 10 kujeruhiwa katika tukio hilo lilitokea katika mkoa wa Kivu Kusini.

Watoto kadhaa "bado hawajapatikana," amebaini padri wa parokia ya Salamabila, Célestin Kijana.

"Kwa ushirikiano na shirika la Msalaba Mwekundu, tumezika miili 18" ikiwa ni pamoja na "watoto wanane", amesema kasisi huyo katika mkoa wa Maniema, hukua kibaini kwamba miili mingi ilikuwa na alama za risasi.

Wanamgambo sita wameuawa na wawili wamekamatwa, kwa mujibu wa Kapteni Dieudonné Kasereka, msemaji wa jeshi la DRC katika Mkoa wa Kivu Kusini, ambaye amebaini kwamba hana taarifa yoyote kuhusu vifo vya raia. Askari mmoja wa FARDC aliuawa na wawili wamlijeruhiwa, ameongezea.

Kwa mujibu wa Shirika la utangazaji la Ubelgiji, RTBF, Jumamosi Januari 11, kulitokea mapigano kati ya askari wa FARDC na wanamgambo wa kundi la Malaika ambao wanadai kulinda masilahi ya wakaazi wanaoishi karibu na mgodi wa dhahabu wa Salamabila.

Kwungiuneko, huko Djugu, katika mkoa wa Ituri, watu wawili wamepoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa, baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa CODECO.

Msemaji wa jeshi la FARDC Luteni Jules Ngongo, amesema makabiliano hayo yalizuka baada ya jeshi kuchukua jukumu la kupambana na waasi hao hasa katika eneo la Tsoro, baada ya waasi hao kuendelea kusababisha hofu ya kiusalama.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana