Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Urusi na Uturuki wakutanisha mahasimu wawili Libya

media Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu (kushoto) na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, katika mkutano wa waandishi wa habari, baada ya kuwakutanisha kwa mazungumzo viongozi wakuu nchini Libya, huko Moscow. © Pavel Golovkin / Pool via REUTERS

Mazungumzo yaliyofanyika Jumatatu wiki hii jijini Moscow kati ya wahusika wakuu katika mzozo wa Libya, kiongozi wa serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, Fayez el-Sarraj, na mbabe wa kivita Mashariki mwa nchi hiyo, Marshal Khalifa Haftar, yamepiga "hatua" bila hata hivyo kufikia makubaliano ya kusitisha vita.

Baada ya mazungumzo hayo, "hatua kubwa imepigwa", amesema Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi.

Kiongozi wa serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa Fayez al-Sarraj, ametia saini mkataba wa makubaliano ya kusitisha vita, lakini mpizani wake, Khalifa Haftar ameomba muda zaidi kupitia makubaliano hayo

Mbabe huyo wa kivita Mashariki mwa Libya , ametoa muda hadi leo Jumanne asubuhi ili kuweza kutia saini yake kwenye nakal hiyo.

Nakala hiyo inabainisha mfumo wa kusitisha mapigano, mchakato ulioanza kutekelezwa Jumapili, Januari 12.

Hata hivyo mazungumzo hayo yaliyolenga kusaidia kuleta amani na kukomesha mapigano nchini Libya, yameahirishwa baada ya pande pinzani kushindwa kuelewana.

Licha ya Marshal Khalifa Haftar kujizuia kutia saini yake, Sergei Lavrov na mwenzake wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu, wamesema wana matumaini kuwa mambo yatakuwa mazuri.

Wakati huo huo Urusi na Uturuki wametoa wito kwa pande zote mbili kukubaliana.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana