Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mkutano wa Pau: Paris na G5 Sahel wakubaliana kupambana dhidi ya makundi ya kijihadi

media Mkutano na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa Pau, Januari 13, 2020. © Guillaume Horcajuelo/Pool via REUTERS

Mkutano wa marais kutoka nchi tano za Ukanda wa Sahel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mji wa Ufaransa wa Pau, umekuwa na matokeo mazuri.

Viongozi wa nchi hizo tano za Ukanda wa Sahel (G5 Sahel) walipokelewa Jumatatu wiki hii na mwenyeji wao, Emmanuel Macron, katika mji huo wa Pau, kwa mazungumzo kuhusu hali inayoendelea katika ukanda huo.

Baada ya mazungumzo yao, marais wa nchi hizo sita walitangaza kwamba walikubaliana kuimarisha ushirikiano wao wa kijeshi. Kama ilivyotakikana na Ufaransa, marais wa nchi za G5 Sahel walielezea msimamo wao kuhusu uwepo wa vikosi vya Ufaransa katika ukanda wa Sahel.

Marais wa nchi za Ukanda wa Sahel wameelezea matakwa yao "kwa Ufaransa kuendelea kutoa ushiriki wake wa kijeshi katika ukanda huo". Wameomba "kuwepo kwa vikosi vya kimataifa kwa kushirikiana na vikosi vyao". Wakuu wa nchi hizo tano pia wamebaini kwamba "wanathamini msaada muhimu wa Marekani" na wana matumaini kwamba msaada huu utaendelea, wakati Washington inafikiria jinsi ya kupunguza vikosi vyake katika ukanda huo.

"Hatua hii ya pamoja, inakusudia kulinda raia, kutetea uhuru wa nchi, kuzuia kuongezeka kwa tishio la kigaidi katika nchi zinazopakana, " wamesema viongozi wa nchi za Ukanda wa Sahel.

Wakuu wa nchi za Ukanda wa Sahel wametangaza kwamba wanataka "kuongeza na kuratibu juhudi zao kwa lengo la suluhisho la haraka katika mzozo wa Libya", ambao wanachukulia kuwa ni chanzo cha kukosekana kwa utulivu katika Ukanda wa Sahel.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana