Pata taarifa kuu
DRC-UN-USALAMA

Ripoti ya UN: Watu 701 wauawa Ituri katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili

Ofisi ya Umoja wa Mataifa na Haki za Binadamu (UNJHRO) imebaini katika ripoti yake kwamba machafuko ya Ituri, tangu Desemba 2017, "yanaweza kukusanya maambo muhimu kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Nyapala, kijiji cha wilaya ya Irokpa, kilishambuliwa na kuchomwa moto Machi mwaka jana, huko Ituri, DRC.
Nyapala, kijiji cha wilaya ya Irokpa, kilishambuliwa na kuchomwa moto Machi mwaka jana, huko Ituri, DRC. © RFI/Florence Morice
Matangazo ya kibiashara

Karibu watu 701 wameuawa," kulingana na ripoti hii kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa na Haki za Binadamu (UNJHRO). Idadi kubwa ya waathiriwa wa shambulio hilo inaonekana kuwa walilengwa kwa sababu ya jamii yao ya Hema.

Karibu watu 402 kutoka jamii hiyo waliuawa kati ya mwezi Desemba 2017 na mwezi Septemba 2019. "

Wakimbizi wamekuwa wakiingia nchini Uganda kupitia ziwa Albert na kuhatarisha maisha yao mara kadhaa.

Mapigano jimboni Ituri yamehusisha jamii ya Hema na Lendu ambao ni wakulima na wafugaji wenye historia ndefu tangu kuanza kwa uhasama wakigombania ardhi kaskazini mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.